Jumuiya ya Qur'an na Sunnah ya Africa ya Mashariki [QSSEA]

Having Problems, follow this link for live stream - LIVE


 
Ni Wakati Gani ‘Amali Ya Mtu Inapokubaliwa?

At-Tawassul

Imebainishwa katika Kitâb na Sunnah yakwamba kwa amali kuwa ni amali njema na iwe ni yenye kukubalika mbele ya Allâh (سبحانه), na iwe ni yenye kumkurubisha mtu karibu na Yeye, basi haina budi kutekeleza masharuti mawili:
LA KWANZA: ni kwamba ni lazima mwenye kuifanya (amali hiyo) awe amekusudia kwa ajili yake, Uso wa Allâh (عزّ وجلّ).
LA PILI: ni lazima iafikiane na vile inavyo-ongoza Sheriya ya Allâh (تبارك وتعالى) katika Kitâb chake au alivyobainisha Mtume Wake katika Sunnah zake. Na iwapo mojawapo ya sharuti hizi mbili imekosekana, basi amali hiyo haitokuwa njema wala haitokubalika. Hii imeashiriwa na maneno yake Allâh (تبارك وتعالى):

فَمَن كَانَ يَرۡجُواْ لِقَآءَ رَبِّهِۦ فَلۡيَعۡمَلۡ عَمَلٗا صَٰلِحٗا وَلَا يُشۡرِكۡ بِعِبَادَةِ رَبِّهِۦٓ أَحَدَۢا
“Kwahivyo yoyote mwenye matumaini ya kuonana na Mola wake, basi na atende amali njema na wala asimshirikishe na yoyote katika waja wake.”

Kwahivyo Yeye (سبحانه) ameamrisha yakwamba amali ni lazima ziwe ‘njema’, yaani ziwe kulingana na Sunnah. Kisha akaamrisha yakwamba zifanywe kwa kutakasiwa Yeye na wala isiwe ni kwa ajili ya motisha yoyote. Amesema al-Hâfidh Ibn Kathîr katika Tafsiri yake: “Mambo haya mawili ndizo nguzo mbili za amali yenye kukubaliwa, ni lazima itekelezwe kwa ajili ya kumtakasia Allâh, na itekelezwe kisawasawa kulingana na jinsi ilivyofundishwa katika Sheriya za Mtume wa Allâh (صلى الله عليه وسلم).” Na amepokea mfano wa haya, Qâdhi ‘Iyâdh (رحمه الله) na wengineo.

MAKALA MAPYA

RIFQAN AHL AS-SUNNAH BI AHL AS-SUNNAH - Sheikh 'Abdul-Muhsin al-Abbaad ‎‎(hafidhahullāh)‎

WASIFU WA SHEIKH ALI IBN HASAN IBN 'ABDULHAMID AL-HALABI - QSSEA‎

NASWAHA YA SHEIKH ABDUL-MUHSIN AL- ABBÂD KWA WANAFUNZI WA KI’ILIMU [TWALABATUL ‘ILM] - Sheikh 'Abdul-Muhsin al-Abbaad ‎‎(hafidhahullāh)‎

NASWAHA YA SHEIKH ABDUL-MUHSIN AL- ABBÂD KWA SHEIKH RABI' BIN HADI AL-MADKHALI (حفظهما الله) - Sheikh 'Abdul-Muhsin al-Abbaad ‎‎(hafidhahullāh)

‎TUNAMUHUKUMU VIPI MTU KUWA NI SALAFI AU SI SALAFI? Sheikh 'Abdul-Maalik ar-Ramadhaani ‎‎(hafidhahullāh)‎

MANHAJ YA ISIS - Sheikh Mash-hur Hasan Āl Salmân (hafidhahullâh)

NI NANI ALIYEMTANGULIA IMÂM AL-ALBÂNI KUHUSU MAKATAZO YA KUFUNGA SIKU YA JUMAMOSI - Sheikh Mash-hur Hasan Āl Salmân (hafidhahullâh)SOMA MAKALA ZAIDI...